Loading...
 

Uundaji wa Klabu- Uanzilishi

 

Kuweni na mkutano wa kwanza.

 

Agora Ambassador Lamichhane Shyam (8th from the right) and the members of the first club in Nepal - Kathmandu Speakers Club
Balozi wa Agora Lamichhane Shyam (wanane kutoka kulia) na wanachama wa klabu ya kwanza nchini Nepal - Klabu ya Kathmandu Speakers

Fanyeni mkutano. Hakikisha unapiga chapa ajenda za kutosha, na haswa kujumuisha kwenye kila ajenda:

  • Taarifa ya klabu yenu na mawasiliano.
  • Tarehe, muda, na mahali pa mkutano unaofuata

Kumbuka kupiga picha, kwasababu mnatengeneza historia, :-) tutumie picha ili tuweze kuzichapa (hakikisha na watu waliopo kwenye picha hizo kama wamekubali zichapwe).

Kwenye mwisho wa mkutano, inapendekezwa kuwa ukumbushe watu tarehe za mkutano unaofuata, waulize watu hapo hapo, na hakikisha unachukua majukumuu ya mkutano ujao.

Maofisa wa Klabu

Baada ya mkutano wa kwanza, ni muda wa kuamua kuhusu Maofisa wa Klabu na Timu ya Usimamizi wa Klabu. Majukumuu ya maofisa wanaohitajika yataelezewa baada kwenye mwongozo huu.

Kwa kawaida, mtu ambaye ameanzisha klabu anatakiwa kuwa rais wa kwanza pia. Baadhi ya watu wanabaki kuwa marais kwa mwaka mmoja mzima, wengine wanapendelea kuanzisha klabu, wanahakikisha kwamba ipo salama na kuondoka madarakani, na kufanya vitu vingine. Inategemea na muda ambao unao.

Kwa maofisa waliobaki, kwa kawaida mwanzoni, utakuwa unafanya majukumuu yote, labda kwa muda wa mwezi mmoja au miwili. Lakini inapendekezwa kuwa uunde timu ambayo unaweza kufanya nayo kazi vizuri na upange kazi haraka iwezekanavyo ili usichoke.

Maofisa wa kwanza wanaweza kuwa maofisa wa kujitolea ambao wewe, kama mwanzilishi wa klabu, umewateua. Pale klabu ikiwa "imara" (mikutano inakuwa mara kwa mara na watu hao hao wanarudi kila mkutano), unaweza ukauliza timu inayofuata wakati wa mkutano maalum wa klabu.

Kama zaidi ya watu wawili wanataka kufanya jukumu moja, uchaguzi lazima ufanyike. 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Wednesday June 2, 2021 12:39:26 CEST by zahra.ak.